Kufuatia uharibifu uliotokea kwenye Uwanja wa Taifa, Oktoba mosi, 2016 wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Simba dhidi ya Yanga, kisha Serikali ya Tanzania kutangaza kuufungia uwanja huo, hatimaye sasa umefunguliwa na ruksa kutumika katika shughuli mbalimbali.
Barua kutoka wizarani kuhusu Uwanja wa Taifa. |
Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ambaye ndiye aliyetoa agizo la kufungiwa kwa uwanja huo na baadaye kuagiza klabu za Simba na Yanga kuingia gharama ya kufanya matengenezo ya uharibifu yaliyotokana na mashabiki wao katika mchezo huo, ametoa tamko la kuruhusu matumizi ya uwanja huo baada ya matengenezo kukamilika.
Kupitia barua kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imeeleza kuwa Waziri Nape ameridhika na ukarabati wa miundombinu uliofanyika kwa gharama za Klabu za Simba na Yanga ambazo zilihusika katika uharibifu huo.
Mashabiki waking'oa viti. |
Waziri Nape akikagua uharibifu uliotokea wiki kadhaa zilizopita. |
Muonekano wa Uwanja wa Taifa kwa juu. |
Waziri Nape amesema ni kursa uwanja huo kutumika kwa michezo na shughuli nyingine za kijamii kuanzia leo Januari 27, 2017 kwa kufuata taratibu zilizopo.
Aidha, Waziri Nape amewatahadharisha wapenzi na wadau wote wa michezo kuutunza uwanja huo na kueleza kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote, klabu au kikundi cha watu watakaohusika katika uharibifu kwa kuwa kuna kamera mpya zimefungwa kwa ajili ya kuimarisha ulinzi.
0 COMMENTS:
Post a Comment