Kocha wa Yanga, George Lwandamina anasifika kwa kuwa mjanja wa kusoma saikolojia ya wachezaji wake.
Lakini Mzambia huyo ana uwezo mzuri wa kushauri wachezaji wake wanapokuwa na matatizo hata yale ya nje ya uwanja.
Alionyesha mfano huo alipotumia muda kadhaa wa kuzungumza na kiungo wake, Deus Kaseke ambaye hakufanya mazoezi jana wakati Yanga ikijifua kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Lwandamina ni kocha mtaratibu lakini anayependa kuona wachezaji wake wakiwa huru na wenye furaha kwa kuwa anaamini watafanya kazi yao kwa ufasaha zaidi.
0 COMMENTS:
Post a Comment