January 26, 2017


Kocha wa makipa wa Simba, Iddi Salim raia wa Kenya amesema juhudi za makusudi zinaendelea kuhakikisha makipa wake wanaboresha kiwango chao.

Salim aliyewahi kuinoa Gor Mahia, AFC Leopard na timu ya tafa ya Kenya, Harambee Stars amesema kiwango walichonacho makipa hao ni bora lakini lazima kukiimarisha zaidi.

"Hii ni kazi ya kila siku, lazima kuboresha kiwango kila siku. Lakini vizuri kuhakikisha kinapanda kila siku," alisema.

Kwa sasa makipa wote wako vizuri, yoyote anaweza kudaka lakini chaguo la mwalimu mkuu (Joseph Omog) linabaki kuwa la kwanza.

"Nashukuru makipa wanafanya kazi yao vizuri na kwa juhudi kubwa kwa kweli," anasema.
Simba ndiyo ipo kileleni mwa Ligi Kuu Bara ikiwa imefungwa mabao 6 tu na kuifanya kuwa na safu ngumu zaidi ya ulinzi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV