Kampuni ya StarTimes Tanzania, leo Jumanne imehitimisha chemsha bongo yake ya Shinda Runinga na Startimes kwa kumpatia runinga ya kisasa mshindi, Tetrino Mkalawa mkazi wa Makumbusho jijini Dar.
Akizungumza na wakati wa kutoa zawadi hiyo kwenye makao makuu ya kampuni hiyo, Mwenge-Bamaga jijini Dar, Afisa Uhusiano wa StarTimes Tanzania, Josephine Stephen, amesema chemsha bongo hiyo imeenda kwa mafanikio makubwa.
“Chemsha bongo hii ilikuwa ikifanyika kila Jumatano saa 2:30 hadi 2:45 usiku kupitia TV1, tunashukuru imekuwa na mafanikio makubwa na kuwapata washindi watano ambao wote tumewakabidhi runinga za kisasa,” alisema Josephine.
Katika hatua nyingine, StarTimes imeahidi kutoa bidhaa bora kwa wateja wao kulingana na mahitaji yao kupitia maudhui yanayoendana na maisha halisi ya Mtanzania kama vile habari, michezo, tamthilia na filamu mbalimbali.
0 COMMENTS:
Post a Comment