January 17, 2017Kocha Mkuu wa Majimaji, Kali Ongala amesema wanataka ushindi dhidi ya Yanga, leo.

Majimaji inaikaribisha yanga katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea.

Kali aliyewahi kukipiga Yanga akutokea Abajalo FC ya Sinza, amesema anataka kuona vijana wake wanashinda.

“Tuko vizuri sana, tumejiandaa ingawa tunajua Yanga ni timu kubwa. Lakini tunataka kushinda kwa kuwa pointi tatu kwetu ni muhimu sana,” alisema.

Kali amesisitiza wako katika wakati mgumu kwa kuwa nafasi ya 14 hadi sasa, si jambo zuri kwao. Hivyo lazima washinde waanze kujikwamua kutoka mkiani.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV