February 3, 2017



Kama unakumbuka, Msemaji wa Simba, Haji Manara amekuwa akisisitiza mechi dhidi ya watani wao, Yanga ichezeshwe na mwamuzi kutoka nje.

Sasa Chama cha Waamuzi Tanzania (Frat) kimempa Manara kazi ya kutafuta atakayeweza kuchezesha mechi ya watani wa jadi Simba na Yanga kwa kufuata weledi ya sheria 17 za soka.

Kwa kuwa watani hao wanatarajia kukutana Februari 25, mwaka huu, maana yake Manara ananafasi kubwa ya kumpata mwamuzi huyo.

Simba na Yanga, zinatarajia kukutana katika Ligi Kuu Bara ambapo awali ilipangwa wacheze Februari 18 lakini mchezo huo umesogezwa mbele kutokana na majukumu ya kimataifa ya Yanga.

Mwenyekiti wa Frat, Mwalimu Nassor, amesema bado hawajapanga ratiba ya mwamuzi wa mechi ya watani.


“Wakati mwingine hatupendi malalamiko, maana kila timu inayofungwa au kuzidiwa ndiyo hulalamika. Basi yeye atafute huyo mwamuzi ili tupunguze lawama," alisema Mwalimu.

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic