February 1, 2017Katibu wa Baraza la Wazee wa Yanga, Ibrahim Akilimali ameibuka na kusema,  mahasimu wao Simba watasubiri sana kuweza kufanikiwa kutwaa ubingwa msimu huu kutokana na tayari wamesharejea katika nafasi yao.


Yanga sasa inaongoza msimamo wa ligi kwa kuwa na pointi 46 ikiwa imeipita Simba pointi moja ambao wana 45 kutokana na kupoteza mchezo wake dhidi ya Azam FC.


Akilimali amesema kuwa, kufuatia kufanikiwa kupanda kileleni mwa msimamo wa ligi timu yao hiyo itaendelea kuongoza hadi mwisho wa msimu na mwisho wa siku kufanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi.


“Yanga sasa ndiyo tumepiga hodi ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu na tutaendeleza kipigo katika kila timu na hatutegemei kurudi nyuma tena hapa ni mbele kwa mbele na tunachokiangalia ni ushindi katika kila mechi.


“Simba ifanye kazi kubwa sana kuweza kutufikia kwani tayari imeshapoteza nafasi, hata Azam hakuna timu itakayoweza kuifikia tena Yanga kwani ndiyo mabingwa


“Yanga ipo vizuri na tumejiandaa kuhakikisha tunafanikiwa kuweza kuchukua ubingwa wa bara na FA, naamini umoja waliokuwa nao wachezaji na viongozi utasaidia katika kufanya vizuri,” alisema Akilimali.


Aidha akizungumzia kuhusu mshambuliaji Obrey Chirwa kufanikiwa kufunga mabao mawili dhidi ya Mwadui, alisema kuwa, yeye ndiye aliyeanza kumponda mchezaji huyo na hatoacha kufanya hivyo pale atakapoona anafanya vibaya kwa kuwa ndiyo mchezaji aliyesajiliwa kwa pesa nyingi katika ligi ya Bongo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV