February 6, 2017




Timu ya Kimondo Super SC imeshushwa madaraja mawili (hadi Ligi ya Mkoa), na matokeo ya mechi zake zote ilizocheza katika kundi la B yamefutwa kwa kushindwa kufika uwanjani kucheza mechi dhidi ya JKT Mlale bila sababu za msingi.

Mechi hiyo namba 47 (JKT Mlale vs Kimondo Super SC),ilitakiwa kuchezwa Januari 28, 2017 kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea, lakini Kimondo Super SC haikutokea uwanjani wala kutoa taarifa yoyote hadi Februari 1, 2017 ilipotuma taarifa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), na kutoa sababu ambazo hazikukubaliwa na Kamati.

Pia Kimondo Super SC imetozwa faini ya sh. 2,000,000 (milioni mbili) ambapo kati ya hizo sh. 1,000,000 (milioni moja) itachukuliwa na TPLB, na sh. 1,000,000 (milioni moja) italipwa JKT Mlale. Adhabu dhidi ya Kimondo Super SC ni utekelezaji wa Kanuni ya 28(1) na (2) ya Ligi Daraja la Kwanza.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic