February 3, 2017



MPIRA UMEKWISHAAAA DAKIKA 3 ZA NYONGEZA
Dk 89, krosi nzuri ya MSuva lakini kipa wa Stand yuko makini hapa
Dk 84, kipa aliyeingia wa Stand anaonekana kuboresha ulinzi vizuri kwenye lango lake
Dk 81, Selembe tena anapata nafasi lakini hakuna anayelifanya
Dk 75 sasa, bado Yanga wanaonekana kutawala zaidi eneo la katikati ya uwanja na kama Stand hawatakuwa makini watatundikwa bao la tano


Dk 69, Juma Abdul anaachia mkwaju mkali hapa lakini unatoka sentimeta chache kwenye lango la Stand
GOOOOOOO Dk 68, Cannavaro anaruka na kufunga kwa kichwa mabeki na kipa wa Stand wakiwa wamesimama kama waliochoka hata kuruka

Dk 64, Yanga wanaingia vizuri hapa la krosi ya Juma Abdul inakosa mwenyeweKADI DK 60 REvocatus Richard analambwa kadi ya njano kwa kucheza kindava
DK 58, Msuva anakwenda kuupiga mkwaju huo........puuuuuuuuuu, anapaisha juu kabisa
KADI Dk 57, Mulilo analambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Msuva
PENAAAAAT Dk 57, Erick Mulilo anamuangusha Msuva na inakuwa penaaaaaaaaaaaaat


Dk 54, inaonekana Stand wamezidiwa na presha kwa kuwa Yanga wanapenya mara nyingi zaidi langoni mwao
Dk 51, Yanga wanalisakama mfululizo lango la Stand United
Dk 47, Selembe tena anaingia vizuri hapa lakini anamgonga Dida wakati wakiwania mpira
GOOOOOOO Dk 45, Chirwa anaingia vizuri kabisa hapa na kuachia mkwaju mkali, bao la tatu




MAPUMZIKO
DAKIKA 4 ZA NYONGEZA

Dk 45, Chiedebere anaingia vizuri, katika ya mabeki wa Yanga, anaachia mkwaju mkali, nje
Dk 43, Chirwa anaingia vizuri, yeye na kipa anaukosa mpira na kuanguka
Dk 39, Yanga wanaendelea kulisakama lango la Stand, hali ilivyo wasipokuwa makini Stand wanaweza kulambwa bao jingine kwa kuwa wanaruhusu krosi kutoka pembeni
Dk 36, Dida alikuwa anatibiwa pale chini baada ya kugongana na Selembe wakati wakiwania mpira. SAsa amesimama


Dk 32, Chidiebere na Selembe wanagongeana vizuri, Selembe anaachia mkwaju mkali kabisa. Goal kick
GOOOOOO Dk 26, Msuva anaingia vizuri na kufunga kwa shuti kali linalogonga nyavu za juu

Dk 23 sasa, Yanga wanazidi kushambulia na Stand wanatakiwa kuwa makini zaidi la sivyo wataoga mvua ya mabao


Dk 19, Yanga wanaingia tena, krosi nzuri ya Juma, hakuna mtu hapa
GOOOOOOO Dk 17, Ngoma anaunganisha vizuri krosi ya Msuva na kuandika bao saafi la kwanza
DK 14, kila upande unafanya mashambulizi lakini ulinzi unaonekana kuwa mkali zaidi kwa kila upande 
Dk 10, Shambulizi jingine wanafanya Yanga kwa mpira wa faulo wa Mwinyi lakini Stand wanaokoa


Dk 7, Selembe anaingia vizuri kabisa baada ya kugongeana na Chidiebere lakini Disa anatoka na kudaka
Dk 5, Yanga inapata kona ya pili baada ya Niyonzima kupiga mpira ukaokolewa na kutoka. Kona yenye haina matunda
Dk 4, Ngoma anaingia vizuri, lakini Stand wanawahi na kutoa inakuwa kona
Dk ya 1 mpira umeanza kwa kasi na Yanga ndiyo wanaoshambulia mfululizo

KIKOSI CHA YANGA
1. Deougratius Munishi ‘Dida’
2. Juma Abdul
3. Mwinyi Haji 
4. Nadir Haroub 
5. Kelvin Yondani
6. Justice Zulu
7. Simon Msuva
8. Thabani Kamusoko
9. Donald Ngoma
10. Obey Chirwa
11. Haruna Niyonzima

Akiba
Ben Kakolanya
Ramadhani Kessy
Vicent Andrew 
Deus Kaseke
Martin Emmanuel

Said Juma Makapu

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic