Ulimwengu ameanza kuitumikia klabu yake ya AFC ya Sweden na kuisaidia kupata sare ya bao 1-1.
Ulimwengu ametoa pasi wakati AFC ikiivaa IF Elfborg ya Sweden pia katika mechi ya kirafiki kujiandaa na Ligi Kuu Sweden.
Timu hizo za Sweden zilikutana katika mechi ya kirafiki mjini Barcelona ambako zimeweka kambi na Ulimwengu akatoa pasi ya bao la kusawazisha katika dakika ya 81 baada ya wapinzani wao kuwa wametangulia kufunga, mapema.
Ulimwengu amejiunga na timu hiyo baada ya kuvunja mkataba wake na TP Mazembe ya DR Congo ambayo alijiunga nayo akitokea AFC pia.
0 COMMENTS:
Post a Comment