March 20, 2017
Kumbuka Mario Balotelli haishi vituko, si unakumbuka alishindwa kuvaa bips?

Safari hii amekosa dakika mvili za mchezo wao Nice dhidi ya Nantes Ligi Kuu ya Ufaransa kwa kuwa alishindwa kufunga kamba.


Hii ilitokea juzi wakati Balotelli akihangaika kukaza kamba za viatu kwa dakika mbili wakati timu yake ikipambana uwanjani.

Alisumbuka hadi mmoja wa maofisa wa Nice akalazimika kwenda kumsaidia.


Tokea ametua Ufaransa pamoja na kufanya vema lakini Balotelli amekuwa akikumbana na mikasa ya kadi nyekundu kutokana na mambo yake ya kushangaza.


Lakini kinachomfanya aendelee kubaki katika kikosi hicho ni ubora wake katika ufungaji.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV