March 20, 2017Kocha wa zamani wa Simba, Zdravko Logarusic amepata usafiri mpya baada ya kukabidhiwa gari aina ya Toyota Tundra.

LOgarusic sasa ni kocha wa Asante Kotoko na uongozi wa klabu hiyo ya Ghana umemkabidhi gari hilo kama sehemu ya mkataba.

“Ndiyo gari ninalotumia nikiwa hapa Accra, ni vizuri kuona watu wanaonyesha kuithamini kazi yako,” alisema.

Hata hivyo, Loga raia wa Croatia alikataa kusema kama gari hilo ni mali yake sasa au sehemu ya mkataba kama matumizi tu.

Kabla kocha huyo alimshukuru mwenyekiti wa Asante Kotoko kwa zawadi ya kushitukiza. 


Baada ya kuondoka Simba ambako alitupiwa virago, Loga alikwenda kwao Croatia lakini baada ya muda mfupi alipata kazi nchini Kenya kuinoa AFC Leopards ambako hakudumu sana, akahamia Angola ambako baadaye aliamua kuondoka mwenyewe na kurejea Ghana.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV