March 21, 2017Himid Mao ndiye nahodha mpya wa kikosi cha Taifa Stars kitakachoshiriki michuano ya Chan, yaani mashindano ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ndani ya Afrika.

Mao, kiungo mkabaji wa Azam FC, atasaidiana na nahodha wa Simba, Jonas Mkude.

Wawili hao watachukua nafasi hiyo ikizingatiwa, nahodha Mbwana Samatta hataruhusiwa kucheza michuano ya Chan kwa kuwa yuko KRC Genk ya Ubelgiji.

Samatta amekuwa akikosa michuano ya Chan kwa kuwa pia alikuwa DR Congo akiichezea TP Mazembe.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV