March 21, 2017

Droo ya Hatua ya Mtoano ya Kombe la Shirikisho Afrika imepangwa leo Jumanne, Shirikisho la Soka la Afrika (Caf) limetangaza kuwa Yanga itacheza dhidi ya MC Alger ya Algeria katika hatua hiyo ya mtoano.

Yanga ilitinga hatua hiyo baada ya kutolewa na Zanaco ya Zambia katika Ligi ya Mabingwa Afrika kwa Zanaco kupata faida ya bao la ugenini kwa kuwa mchezo wa kwanza ulimalizika kwa sare ya bao 1-1 jijini Dar es Salaam kisha kutola suluhu waliporudiana nchini Zambia.

Wakati Waarabu hao wapo hatua hiyo baada ya kuiondoa Renaissance du Congo yaDRC katika hatua iliyopita ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Mechi ya kwanza inatarajiwa kuchezwa kati ya Aprili 7 hadi 9, mchezo wa pili utapigwa kati ya Aprili 14 hadi 16, mwaka huu

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV