April 4, 2017KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, jana asubuhi ilifanya ziara kwa wadhamini wake wakuu Benki ya NMB, ambayo imeonyesha kuridhishwa na udhamini wake kwa mabingwa hao. Azam FC imetumia ziara hiyo kujifunza mambo mbalimbali yaihusuyo benki hiyo inayoongoza nchini kwa sasa, ikiwemo kuwapelekea makombe matatu waliyopata kipindi cha udhamini wa NMB kuanzia msimu wa 2014-2015 ilipoanza hadi sasa.

Akizungumza wakati wa kuikaribisha timu hiyo, Afisa Mkuu wa Fedha NMB, Waziri Barnabas, alisema kuwa wanayofuraha kubwa kuendelea na udhamini wao kwa Azam FC huku akiipongeza kwa mafanikio wanayoendelea kuyapata na kuwaomba waendelee kuongeza juhudi.
“Leo sisi ni furaha kuwaona wachezaji wakiwa hapa, tunawapa hongera sana kwa mafanikio mnayoendelea kupata, na muendeleze juhudi tunatarajia makubwa kutoka kwa Azam na tunaona itakuja kuwa ni timu ambayo ni ya mfano Tanzania na Afrika kwa ujumla, kwa hiyo hongera mnayo sapoti yetu kwa ujumla, tunafuraha sana leo mmeweza kutuletea baadhi ya makombe ambayo mmepata na wafanyakazi wetu wamefurahi kuwa pamoja na nyie,”

Naye Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba akiongea kwa niaba ya Bodi ya Wakurugenzi ya Azam FC aliushukuru uongozi wa NMB kwa kuendelea na udhamini huo huku akidai kuwa kupitia ushirikiano wao wamefanikiwa kutimiza mambo mengi ya maendeleo ya timu hiyo.

“Huu udhamini tunaouzungumza ni ushirikiano ambao umetusogeza sana na Azam FC na tunaamini kabisa kwamba baada ya muda mfupi watu wengine wanaweza kuuliza kwamba kwanini Azam FC na sio wengine? Lakini siri ni moja tu kutengeneza mfumo wako mzuri, kila kitu kiwe na uwazi, uwajibikaji uwe unaonekana, halafu baada ya hapo watu watakuja kufanya kazi na wewe,” alisema.
Kwa mara ya kwanza NMB kuipa udhamini Azam FC ilikuwa ni mwanzo mwa msimu wa 2014/15 ukiwa ni wa miaka miwili baada ya kutwaa taji la kwanza la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) 2013/14 kwa rekodi ya kutopoteza mchezo wowote, udhamini ambao umeongezwa tena msimu huu.


<iframe width="853" height="480" src="https://www.youtube.com/embed/Jz8dbQ-TUbQ" frameborder="0" allowfullscreen></iframe> 


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV