April 21, 2017


Celta Vigo imepata safe ya bao 1-1 dhidi ya Genk ya Ubelgiji ambayo anaichezea Mtanzania Mbwana Samatta.

Sare hiyo inaivusha Celta hadi nusu fainali ya Europa League kwa kuwa mechi ya kwanza nyumbani ilishinda kwa mabao 3-2.

Juhudi za Samatta kuhakikisha Genk inasonga mbele dhidi ya timu hiyo ya Hispania, ziligonga mwamba.

Mechi hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Cristal Arena ilikuwa ngumu na Celta walianza kupata bao katika dakika ya 63 kupitia Pione Sisto lakini wenyeji wakasawazisha kupitia Leandro Trossard.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV