April 20, 2017



Na Mwandishi Wetu, China
Kwa miaka ya hivi karibuni, ulimwengu wa soka umeshuhudia mapinduzi makubwa yaliyoletwa na uwekezaji wa hali ya juu wa  fedha nyingi  kupitiliza;hii imefanya vijana wadogo kununuliwa na kulipwa mishahara mikubwa kuliko vipaji vyao wenyewe.

Wakati dunia ikiendelea kushangaa pesa waliyonunuliwa Paul Labile Pogba,Gonzalo Higuain,Gareth Bale,John Stones,Raheem Sterling na wengine wengi, wachina wao  ndo kwanza kila  kukicha wanavunja benki na kuwatunuku watu hundi kubwa pasi na mifano na  ndo sababu kubwa kwa nini hivi karibuni  tumeshuhudia  majina makubwa yakitoka klabu kubwa na ligi bora kokote kule  duniani na kwenda  China.

Zamani tuliamini na kuona wachezaji ambao umri  umewatupa  kama kina Anelka,Drogba, Xavi n.k ndo wangekata kauli kuja kucheza ASIA KAMA Dubai,Qatar,Oman ila leo imekuwa tofauti wachezaji wa umri mdogo na tena ambao walikuwa na nafasi ya kutengeneza historia kubwa  kwenye ramani ya mpira ulaya kama Oscar, Paulinhno, Axel Witsel, Jackson Martinez,Graziano Pelle, Olunga na wengine wengi wakija CHINA kwa nguvu ya  pesa za usajili na mishahara minono wanayotoa wachina.

Ni wazi vijana wengi watakimbia ulaya kuja huku,na yote hii wanafanya kwa agizo la raisi wao mheshimiwa Xi Jinping ambaye duru lake linataka kufikia 2050, China iwe inaongoza katika viwango vya FIFA katika mpira wa miguu,japo kwa maono na mtazamo wangu hawauhitaji 2050, bali watahitaji kuwa na subira hadi 2025 tu, kufikia hapa na imani dunia itashuhudia mapinduzi makubwa katika ligi ya China.



Si lazima wawe wanaongoza katika viwango vya Fifa vya dunia bali tu hii ligi itakuwa imepewa jicho la dunia, itapata wawekezaji wengi na taswira pana ya kibiashara kama ilivyo ligi ya Uingereza, vijana wengi watajenga kiu ya kutaka kucheza huku na hadi ikifka 2050, China itakuwa imepiga hatua kubwa kimpira kama mataifa mengine kama Uingereza, Hispania, Ufaransa n.k.


Kwa kuyaelewa haya,Watanzania waishiyo China wakaamua kuanzisha timu yao  maarufu kama TANZANIA STARS FOOTBALL CLUB(T.S.FC).

TANZANIA STARS FOOTBALL CLUB(T.S.FC):
T.S.FC ni kifupi cha TANZANIA STARS FOOTBALL CLUB 
Ni taasisi ya kukuzia vipaji inayojitegemea iliyoanzishwa na watanzania wachache wanaosoma Kaskazini mwa China katika jimbo la Liaonning, mji wa Shenyang; mji mkongwe katika historia ya China. Ni saa tano tu kwa treni ya umeme (bullet) kutoka mji mkuu wa China, Beijing na pamepakana na Korea Kaskazini.                                                    

HISTORIA FUPI YA T.S.FC
Ni taasisi inayojihusisha na kukuza vipaji vya mpira wa miguu.Taasisi hii ilianzishwa tarehe  1/11/2013 katika chuo kikuu maarufu hapa Shenyang, SHENYANG AEROSPACE UNIVERSITY (S.A.U).Suala la kuanzisha taasisi lilikuja kama wazo baada vijana watano; ABDULWAHID ISMAIL BITEGEKO, NASSOR KOMBO, HAGGAI JAMES,YUSUPH ISMAIL BITEGEKO na AGGREY JOSEPH MWAKASITA kukaa  chini na kuona kuna haja ya kuanzisha taasisi hii.

Ilianza na wachezaji 10 tu na kwa mtiririko huu ndo taasisi imepiga hatua hadi hapa ilipo hivi sasa. Mpaka kufikia mwaka 2012,hiki chuo SHENYANG AEROSPACE UNIVERSITY (S.A.U) ambapo ndo kila kitu kilipoanzia Kulikuwa na watanzania wawili tu ambao wote hawakuwa wakipenda mpira na ikawalazimu watu wa hapa kusubiri hadi mwaka 2013.

Wakati watanzania walipoanza kuja huku rasmi hususani Kaskazini mwa China hasa ukizingatia Watanzania na wageni wengi wanaokuja China hupendelea kwenda Kusini mwa China kwenye miji kama Guangzhou,Shanghai n.k 


Haikuwa safari rahisi kuisimamisha hii taasisi leo ilipo na hasa ukizingatia kwa kipindi hicho,mwaka 2013,bado masuala ya mpira kwa watu weusi hayakuwa yakipewa kipaumbele kuanzia na vyuo hadi na mji huu,bado wagheni hasa waafrika walikuwa wakiathiriwa na ile dhana ya kuwa mtu mweusi alikuwa bado binadamu mgeni huku.

Hakukuwa na mazingira sahihi ya kuanzisha taasisi ya kimpira huku ikabidi kupiga moyo konde na kwa mapenzi ya mchezo huu pendwa duniani tena wakiwa 10 tu,ikaanzishwa taasisi ya mpira wa miguu ambayo kwa kipindi kile ilionekana kama kitu kigeni sana hata kwa wanafunzi wenzao wa kigeni ambao wengi walikuwa wabezaji na wakosoaji tu. 

Wengi watashangaa kivipi na wachezaji 10? Wachezaji 10 na kipa tulikuwa tunakodisha kutoka kwa  nchi zingine na hawa Watanzania 10 hawakuwa wote wakitokea chuo cha SHENYANG AEROSPACE UNIVERSITY (S.A.U),wengine walitoka karibu kama SHENYANG MEDICAL COLLEGE na CHINA MEDICAL UNIVERSITY. Mwanzoni walicheza mechi za kirafiki na timu za vyuo kwa jua mataifa mengi hayakuwa yamejipanga kwa wakati huo.

Baada ya kucheza michezo kadhaa ndo mataifa kama Nigeria,Ghana,Zambia,Russia na wengine walipofuatia baada ya kuona  ni kwa kiasi gani tumefanikiwa. Mwaka wa 2014 ulikuwa wa matunda mengi na ndipo hii timu ndogo ilipozaa taasisi baada ya kupata vijana wengi ima waliokuja kusoma au hata kuishi huku, ambapo mpaka sasa taasisi imekuwa na ina wachezaji yapata 60 ikiwa na uongozi wa juu, kocha, benchi zima la ufundi wakiwemo madaktari na washabiki wengi tu ambao wote wanafanya kazi kwa ajili ya kujitolea na kwa hisani ya taifa mama la Tanzania.
                                                       

MAFANIKIO YA TAASISI HII;
  • Imekuwa taasisi ya kwanza ya mpira ya waafrika kuanzishwa na kujisimamia yenyewe.Imeweza kusimamia watanzania yapata 60 na wachezaji takribani 12 kutoka Kenya, Rwanda, Burundi, Uganda, Djibouti, Somalia .
  • Japo si kitega ajira rasmi ila tumeweza kutoa ajira zisimo rasmi kwa wachezaji wetu kwa kupata timu za kuchezea hususani za wachina na nchi zingine ambao wamekuwa wakikodi wachezaji kutoka hapa kwa malipo wanayopewa wachezaji wao wenyewe.
  • Tumeanzisha mashindano ya MATAIFA AFRIKA na KOMBE LA DUNIA ya huku kwa hisani yetu wenyewe ambayo kwa mafanikio kabisa yametimiza miaka miwili Tangu kuanzishwa na mara zote tumekua washindi wa pili.
  • Tumeitunza heshima ya Tanzania na leo kila mmoja anajivunia kile wanachofanya watanzania huku na tumechaguliwa kuwa TAASISI BORA YA MICHEZO mara mbili na jumuiya ya watanzania wanaoishi CHINA chini ya UBALOZI WA TANZANIA NCHINI CHINA.
                                                                                  Moja ya mashindano yaliyoandaliwa  na taasisi ya T.S.FC 
DIRA YA TAASISI;
     Dira kuu ya taasisi ni kuifanya hii taasisi kuwa moja ya taasisi kubwa siku za usoni,kuipeleka timu kushiriki LIGI kuanzia madaraja ya chini hadi ligi kuu na pamoja na kuwa kitovu kikuu cha kuwapa nafasi vijana wa kitanzania kuonyesha uwezo wao na hata kupata timu za kwenda kufanya majaribio. 

KWA MAWASILIANO
 whatsapp +8615566140449
Instagram; tanzaniastars
Email; tanzaniastars@gmail.com


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic