April 9, 2017

RAIS WA TFF, JAMAL MALINZI


MKUTANO MKUU WA TFF

Kikao cha Kamati ya Utendaji cha Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), kimekutana  leo Jumapili Aprili 9, 2017 na miongoni mwa maamuzi yake kikao kimeamua kuwa Mkutano Mkuu wa TFF, utafanyika Jumapili ya Agosti 12, 2017.

Miongioni mwa ajenda katika mkutano huo, itakuwa ni uchaguzi mkuu wa TFF. Kwa mujibu wa Katiba, uchaguzi huo utachagua Rais wa TFF, Makamu Rais wa TFF na Wajumbe wa Kamati ya Utendaji.


…………………………………………………………

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV