April 26, 2017



Kauli ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe kutaka maelezo baada ya Yanga kupeleka timu B katika mechi ya kirafiki dhidi ya kombaini ya majeshi, imezua gumzo kubwa mitandaoni.


Dk Mwakyembe ametaka maelezo hayo baada ya Yanga kupeleka kikosi B katika mechi hiyo iliyoisha kwa sare ta bao 1-1 kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma ikiwa ni mahsusi kwa ajili ya sherehe ya muungano.


Lakini mashabiki wengi mtandaoni wameonyesha kukerwa na kauli hiyo na wengi wamekuwa wakimhoji Dk Mwakyembe kwamba hajui Yanga ina michuano muhimu zaidi ya mechi hiyo ya kirafiki.


Mashabiki wengine, wameutaka uongozi wao kukaa kimya na kuachana kabisa na kutoa ufafanuzi, huku wengine wakisisitiza, inawezekana Dk Mwakyembe anapaswa kuanza kufuatilia mchezo wa soka kwa karibu ili kujua nini kinaendelea.

Yanga inakabiriwa na mechi ya Kombe la Shirikisho hatua ya nusu fainali na itacheza Jumapili dhidi ya Mbao FC, mjini Mwanza.


Baada ya hapo, ina michezo kadhaa ya kiporo ya Ligi Kuu Bara ambayo imetokana na Yanga kuwa na michuano ya Kombe la Shirikisho la Caf kabla ya kung’olewa na MC Algers.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic