April 18, 2017Mambo yamezidi kupapamba moto katika Kikao cha Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Kikao hicho kinafanyika katika hoteli ya Protea jijini Dar es Salaam na uongozi wake umezuia makomandoo wa Yanga na Simba kuingia katika eneo hilo.

Tayari maofisa wa Kagera Sugar pia Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geofrey Nyange 'Kaburu' waliingia kuhojiwa.

Baada ya hapo, kikao hicho kimekuwa kikiendelea na huenda baada ya saa moja au mawili kinaweza kufikia tamati.

Kagera Sugar wamepinga Simba kupewa ponti tatu na mabao matatu kupitia Kamati ya Saa 72 iliyobaini beki Mohamed Fakhi alikuwa na kadi tatu za njano.

Tayari imeelezwa majibu yatatolewa leo saa 11, lakini tayari zaidi ya saa moja sasa.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV