Mashabiki wa Arsenal wanaonekana hawajachoka na vita yao ya kuhakikisha Kocha Arsene Wenger anaondoka.
Kumekuwa na kampeni zinazoendelea bila kuchoka zinazofanywa na mashabiki hao wakitumia kauli mbiu ya 'Wenger Out’.
Wamekuwa wakiweka mabango katika sehemu mbalimbali yakiwemo yale ya taa yanayowaka usiku.
Baadhi wameweka mabango hayo kwenye Uwanja wa zamani wa Arsenal wa Highbury pia uwanja wa sasa wa Emirates wakisisitiza kuondoka kwa Wenger.
Kama hiyo haitoshi, mashabiki hao wameanza kuweka kauli mbiu yao mitandaoni wakitumia picha hizo kusisitiza Wenger awaachie timu yao.
0 COMMENTS:
Post a Comment