April 29, 2017

MKEMI

Siku moja baada ya Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB) kumshitaki kwa Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, Salum Mkemi, ameibuka na kusema kesho hatofika kusikiliza shitaka lake kwani ana majukumu ya timu yake.

Mkemi alitakiwa kufika mbele ya kamati hiyo kesho Jumapili katika Ofisi za TFF saa 5 asubuhi baada ya kushutumiwa kwa kuidhalilisha Kamati ya Saa 72, kuwa inaendeshwa kwa unazi na imegubikwa na rushwa katika kushughulikia suala la kadi tatu za njano kwa mchezaji wa Kagera Sugar, Mohammed Fakhi.

 Mkemi alisema: “Sitaweza kwenda kusikiliza nilichoitiwa katika siku hiyo ya Jumapili kwani nipo Mwanza na timu na ndiyo kiongozi wa msafara.

“Tunacheza na Mbao hiyo Jumapili hivyo nimeandika barua kwa TFF kuwataarifu kuwa sitoweza kufika siku hiyo kama kamati ilivyonitaka hivyo wanipangie siku nyingine.

“Mimi sio mualifu isipokuwa ni tuhuma tu juu yangu hivyo ninatakapopangiwa siku nyingine nitakwenda na wamekubali ombi langu hilo.”

Hata hivyo, alipotafutwa Mtendaji Mkuu wa TPLB, Boniface Wambura simu yake iliita bila kupokelewa. Juzi Wambura alitoa taarifa ya Mkemi kutakiwa kwenda kujieleza mbele ya Kamati ya Nidhamu kwa kosa la kuishambulia Kamati ya Saa 72.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV