April 22, 2017



Yanga jana ilifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, na muda mwingi winga Simon Msuva alionekana akipewa mazoezi ya kupiga kona zinazoelekea moja kwa moja wavuni.

Shiza Kichuya wa Simba, amewahi kuifunga Yanga bao la kona ya moja kwa moja Oktoba mwaka jana, katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliozikutanisha timu hizo uwanjani hapo na kutoka sare ya bao 1-1.

Kocha Msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi katika mazoezi hayo alionekana akimnoa Msuva kupiga kona hizo zinazoelekea nyavuni zenyewe ikionekana ni maandalizi ya mechi ya leo dhidi ya Prisons.

Yanga inacheza na Prisons mechi ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho maarufu kama Kombe la FA, leo kwenye Uwanja wa Taifa na mshindi ataungana na Simba, Azam FC na Mbao FC katika nusu fainali.


Wakati Mwambusi akitoa maelekezo yake kwa Msuva kuhusu upigaji huo wa kona, Kocha Mkuu wa Yanga, George Lwandamina alikuwa akifuatilia kwa umakini zoezi hilo.



Baada ya kumaliza mazoezi hayo, Mwambusi amesema kuwa; “Haya ni mazoezi ya kawaida tu kwa Msuva, tuna mechi nyingi muhimu mbele hii ni moja ya mbinu za ushindi.”

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic