April 30, 2017


Aliyekuwa Mkurugenzi wa Habari wa Yanga, Jerry Muro amesema Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limefanikiwa kuwagawanya Simba na Yanga na sasa linawatawala linavyotaka bila kufuata kanuni.

Muro amesema TFF imekuwa ikifungia wadau hasa wale wanaojaribu kuueleza ukweli uongozi wa shirikisho hilo unapokuwa si sahihi.

“Hii nilisema tokea mwanzo, kwamba tushirikiane. Lakini Simba hawakunielewa na waliendelea kufurahia mimi kufungiwa kwangu.

“Sasa Yanga nao wanafurahia kufungiwa kwa Manara. Wamefanikiwa kutugawanya na wanaendelea kututawala wanavyotaka, hii si sahihi.

“Kitu kibaya zaidi TFF wanaendelea kuishi wanavyotana na wana uhakika wa kurejea tena ili waendelee kufanya wanavyotaka.

“Hii si sawa na maendeleo ya mpira wa Tanzania hayana uhakika tena, nawashauri ndugu zangu tuungane kuhakikisha kuna mabadiliko.

“Kuna mambo ya ushindani na kuna mambo ya kushirikiana pamoja na kufanya mambo kwa ajili ya mpira wa Tanzania. Tusiwape nafasi watu wanaotuvuruga waendelee kututawala wanavyotaka,” alisema.

TFF imeendelea kuwafungia wanamichezo wote wanaoonyesha nia ya kuikosoa kwa nguvu hasa pale inapofikia kuendesha mambo kienyeji.


Malalamiko yamezidi kuongezeka kadiri siku zinavyosonga mbele  lakini TFF wanaonekana kutosikiliza huku wakiendelea kuwaadhibu wadau mbalimbali kwa matakwa yao binafsi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic