April 30, 2017

TANO BORA YA WANAMICHEZO TAJIRI UINGEREZA

Baada ya kuingiza kitita cha pauni milioni 15 kutokana na ushindi wa jana, bondia Anthony Joshua, anaonekana anaanza kujivuta kwenye listi ya wanamichezo matajiri duniani.

Joshua alimtwanga mkongwe Wladimir Klitschko katika pambano kali la ngumi za kulipwa, imemuingizia kitita cha pauni milioni 15 ambazo ni Sh bilioni 42.5.

Hata hivyo, Lewis Hamilton, anaendelea kuongoza akiwa na kitita cha zaidi ya pauni milioni 100 kwa mwaka.

Anafuatiwa na nahodha wa Man United, Wayne Rooney anayeingiza kitia cha pauni milioni 85 kwa mwaka wakati mcheza tenisi nyota zaidi wa Uingereza, Andy Murray anapata pauni milioni 60 kwa mwaka.

Kutokana na umaarufu alionao, kama Joshua atapigana pambano jingine, ana uhakika wa kupanda haraka.

Kwani pamoja na fedha za mapambano, wadhamini huongezeka kwa kasi kubwa kutokana na umaarufu wa mwanamichezo.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV