May 1, 2017


Pamoja na kupoteza pambano lake dhidi ya bondia Anthony Joshua, mkongwe Wladimir Klitschko ameendelea kuonyesha yeye ni mtu ‘simpo’ alipoonekana mitaani akiwa na mpenzi wake.


Siku moja tu baada ya kupoteza pambano hilo kwa TKO katika raundi ya 11, Klitschko, 41, alikuwa mtaani jijini London akiwa na mpenzi wake Hayden Panettiere kwa ajili ya matembezi na kupata chakula.

Akiwa mtaani aliwapokea mashabiki kadhaa waliotaka awasainie katika mashati yao na vifaa vingine, naye alifanya hivyo.

Baadaye aliingia katika mgahawa wa Roka ulio West London ili kupata chakula.
0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV