May 20, 2017



Huku Bingwa wa Ligi Kuu Bara akitarajiwa kupatikana leo, Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB) imeandaa makombe mawili kwa ajili ya kumkabidhi bingwa, moja lipo Dar es Salaam na lingine lipo Mwanza.

Kombe moja leo litakuwepo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ambapo Simba inacheza na Mwadui FC ya Shinyanga na lingine litakuwa Mwanza kwenye Uwanja wa CCM Kirumba ambapo Yanga inacheza na Mbao FC. 

Yanga na Simba zote zinawania ubingwa lakini Yanga ndiyo yenye nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa rasmi kwani ina pointi 68 kileleni wakati Simba ni ya pili ikiwa na pointi 65.

Ili Yanga iwe bingwa inahitaji sare hata kufungwa idadi ndogo ya mabao, wakati Simba itahitaji ushindi wa mabao 12-0 huku ikiiombea Yanga kipigo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura amesema wameandaa makombe mawili moja litakuwepo Uwanja wa Taifa na lingine CCM Kirumba, Mwanza. 

“Tumejiandaa kuhakikisha bingwa atakayepatikana kesho (leo) anakabidhiwa kombe lake mara baada ya mechi kumalizika.

“Bado bingwa hajajulikana kati ya Simba na Yanga na mechi zao za mwisho wanacheza kwenye viwanja tofauti, hivyo ni lazima tuandae makombe mawili.


“Hivyo, tayari tumeyaandaa makombe mawili kati ya hayo moja tutalikabidhi kwa bingwa atakayelichukua kati ya Simba na Yanga,” alisema Wambura bila ya kutaka kufafanua kuhusu utaratibu huo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic