May 3, 2017


Kipa Gianluigi Buffon amecheza mechi ya 100 ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na kufanikiwa kumaliza kwa mafanikio.

Katika mechi ya 100, Buffon kipa mkongwe zaidi nchini Italia, ameingoza Juve kuitwanga AS Monaco kwa mabao 2-0.

Juve imeishinda Monaco 2-0 pamoja na kuwa ugenini na mechi ya pili, inaonekana haitakuwa ngumu sana kwake kwa kuwa itakuwa nyumbani.


Hata hivyo, mpira hauna nyumbani wala ugenini na Juve wanapaswa kuwa makini licha ya kwamba watakuwa chini ya safu bora ya ulinzi itakayoongozwa na Buffon.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV