Anthony Joshua ameeleza kile alichokuwa akizungumza na Wladimir Klitschko ambaye alimshinda katika raundi ya 11.
Joshua alionekana akizungumza jambo wakati akiendelea kuzichapa na Klitschko katika raundi ya sita.
Bondia huyo raia wa Uingereza amesema walibadilishana maneno na Klitschko wakati wakiendelea kuzichapa.
“Nilimuambia kama utaniachia nipite raundi hii, basi ujue umekwisha. Naye akajibu kwamba ni lazima atanitwanga na kuniagusha,” alisema Joshua.
Joshua alikuwa wa kwanza kumchapa konde Klitschko akalamba sakafu katika raundi ya tano. Lakini raia huyo wa Ukraine naye akarejea na kumtwanga Joshua konde katika raundi ya sita lililomlazimisha kwenda chini.
0 COMMENTS:
Post a Comment