Kikosi cha JKT Ruvu, kimekiri kwamba kweli kwa sasa kwao ni “maji ya shingo”.
JKT ndiyo timu inayoshika mkia katika Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 23 huku ikijaribu kutumia nguvu kubwa kujikomboa.
Meneja wa JKT Ruvu, Pascal Simbi amesema wanajua kuwa wako katika nafasi ambayo wanalazimika kufanya kazi ya ziada kwa juhudi za juu.
“Tunatakiwa kuwa na juhudi kubwa sana kwa kweli. Tunajua hali yetu si nzuri lakini hatujakata tamaa.
“Tunajua hili jambo linamuumiza kila mmoja wetu. Lakini tutapambana na kubadilisha mambo,” alisema.
JKT Ruvu imeonyesha kuyumba na kutofanya vizuri tokea mwanzo wa ligi hiyo.
Katika mechi 27 ilizocheza, imeshinda tatu tu, imepoteza 10 na sare 14 ikiwa imefunga mabao 14 na kufungwa 24.
0 COMMENTS:
Post a Comment