May 4, 2017
Kiungo wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, Himid Mao, amemuambia rafiki yake wa karibu kwamba ni mapema yeye kuanza kupima atafanyaje katika majaribio yake nchini Denmark.

Himid anafanya majaribio ya siku 10 katika klabu ya Randers inayoshiriki Ligi Kuu nchini Denmark.

Rafiki wa karibu wa Himid, ameiambia SALEHJEMBE kwamba ana imani atafanya vizuri ingawa anahitaji kuona kwanza.

"Himid anajiamini sana, anajua soka kokote linawezekana na amecheza mechi nyingi za kimataiafa. Anajua kuna tofauti lakini soka ni soka.

"Lakini anaona ni mapema kuanza kufikiri itakuwaje, atafuzu au la! Amesema ni vizuri kuendelea na majaribio lakini mapema sana kulijadili suala hilo," alieleza rafiki yake huyo.

Klabu ya Azam FC, imempa Himid baraka kufanya majaribio hayo ya siku 10.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV