May 4, 2017



Kikosi cha Simba kimeingia kambini jijini Dar es Salaa, tayari kuanza kazi ya kuiwinda African Lyon.

Simba itashuka dimbani kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam katika mechi yake ya Ligi Kuu Bara.

Mratibu wa Simba, Abbas Ally ‘Gazza’ amesema wameanza kambi rasmi.

“Sasa tumeanza kambi, imeanza leo. Hii ni sehemu maandalizi ya mechi za mwisho ligi kuu,” alisema.

Taarifa zinaeleza, Simba wamejichimbia Mbweni nje ya jiji la Dar es Salaam na kambi hiyo imeanza rasmi jioni hii.


Katika mechi ya mzunguko wa kwanza, Simba walilala kwa bao 1-0 ukiwa ndiyo mchezo wa kwanza Simba kupoteza.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic