May 1, 2017
Kiungo mshambuliaji wa Simba, Shiza Kichuya, amesema kuwa hatakiwi kutupiwa lawama kwa kushindwa kucheka na nyavu kutokana na ‘ukata’ huo kutomganda peke yake, kwani hata kinara Simon Msuva wa Yanga, naye ameshindwa kufunga kwenye mechi zao.

Kichuya, mwenye mabao 11 kwenye mzunguko huu wa pili, ameifungia timu yake bao moja tu kwenye mechi 12 mpaka sasa, tofauti na mzunguko wa kwanza ambapo alifanikiwa kufunga mabao 10 kwenye mechi 15.

Kiungo huyo wa zamani wa Mtibwa Sugar amesema kuwa kushindwa kwake kufunga kunatokana na ugumu wa ligi ambayo imebakiza mechi tatu ambapo kila timu inakuwa inacheza kwa tahadhari kuhakikisha kwamba haifungwi.

“Ligi imekuwa ngumu na tunakutana wakati mgumu hasa kwenye mechi hizi za mwisho, ndiyo maana unaona spidi yangu ya kufunga imepungua tofauti na ilivyokuwa awali.


“Lakini siyo mimi peke yangu ambaye sijafunga hadi sasa, hata Msuva anayewania tuzo ya ufungaji bora amekomea hapo na mabao yake 12 tofauti na mwanzo, jambo hilo linaonyesha kwamba kuna ugumu kiasi gani kwenye suala zima la kucheka na nyavu,” alisema Kichuya.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV