May 2, 2017

MALINZI (KUSHOTO) AKIWA NA WAZIRI MKUU MSTAAFU, EDWARD LOWASSA


Mashabiki wa Simba wamecharuka baada ya Rais wa TFF, Jamal Malinzi kutupia mtandaoni akieleza droo ya upangaji sehemu ya mechi ya fainali ya Kombe la Shirikisho itafanyika ndani ya siku chache.

Malinzi ameeleza kwamba fainali itakuwa ni Mei 28 lakini droo itafanyika ndani ya siku chache.

Mashabiki wengi wanaoonyesha kuwa ni wa Simba, wamelalamika kwamba Malinzi anawafanyia figisu.

Wengi wamekuwa wakilalamika kwamba TFF imeanza kufanya figisu.

Lakini wengi walionyesha kushangazwa na kufanyika droo ili kupanga sehemu ambayo mechi itachezwa siku ya fainali.


Kwa kawaida mashaindano yote ya mtoano, siku ya fainali huwa inajulikana itachezwa katika uwanja upi wakati mwingine bila ya kujali timu zinatokea wapi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic