May 2, 2017



Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limesema linaendelea na uchunguzi kuhusiana na lile tukio la kishirikina lililofanywa na mwanachama wa Simba.

Mwanachama wa Simba aitwaye Ngade Ngalambe, aliingia na kumwaga kimiminika ambacho baadaye kilielezwa kuwa ni mafuta ya nguruwe.

Alifanya hivyo muda mchache kabla Simba haijaivaa Azam FC katika mechi ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho na Simba ilishinda kwa bao 1-0.

Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas amesema bado wanachunguza na baada ya hapo watachukua hatua.

“Tunaendelea kulifanyia uchunguzi suala hilo na endapo itabainika basi kanuni zipo wazi, hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi ya Simba na aliyefanya kitendo hicho,” alisema Alfred.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic