May 12, 2017


MPIRA UMEKWISHAAAA
-Mavugo anamchambua kipa, lakini anashindwa kufunga baada ya Ibrahim Job kuokoa kabla haujavuka mstari na kwua kona ambayo haina manuvaa kwa Simba

DAKIKA 2 ZA NYONGEZA
Dk 89, shambulizi la Simba linazaa kona, inachongwa hpa lakini haina faida
Dk 86 sasa, kila timu inaonekana kumiliki mpira kwa utulivu sana na Simba wanataka kufunga la tatu wamalize kazi huku Stand wakitaka kusawazisha
Dk 84, Stand wanapata kona baada ya kufanya shambulizi kali
SUB DK 83 Rajab Rashid anaingia kuchukua nafasi ya Aaron Lulambo Upande wa Stand
Dk 81, Simba wanapoteza nafasi ya wazi ya kufunga, Muzamiru yeye na nyavu, krosi safi ya Mavugo
SUB Dk 79, Abdi Banda anaingia kuchukua nafasi ya Kichuya, maana yake, Kotei anakwenda kucheza juu na Banda anachukua namba sita kusaidiana ulinzi na Mkude, maana yake Simba watakuwa na viungo wawili wa ukabaji na hii inaonyesha wamelenga kujilinda zaidi, wakipatia sawa, wakikosea, hatari kwao
Dk 78 anapoteza nafasi nzuri kabisa ya kufunga bao akiwa karibu kabisa na lango la Stand
Dk 77 Kwa hali ilivyo, Simba wanapaswa kuwa makini kwa kuwa wamerudi nyuma, hawakai sana na mpira na muda mwingi Stand United wanashambulia zaidi
Dk 74 Mavugo anaachia mkwaju mkali, unamtoka kipa lakini anawahi kuudaka tena
Dk 72, mpira mzuri wa krosi, Miraji Maka kidogo autumbukize kwenye nyavu za Simba
Dk 69,Stand wanaonekana kuwasumbua zaidi Simba hasa katika upangaji wa mashambulizi
Dk 66, nafasi nyingine nzuri kwa Kichuya lakini shuti lake linaishia mikononi mwa kipa wa Stand
Dk 63 Liuzio mfungaji wa mabao mawili ya Simba anakwenda benchi na basi yake inachukuliwa na Pastory Athanas


Dk 61 Juuko anafanya kazi ya ziada kuokoa krosi safi ya Stand na kuwa kona. Wanachonga kona, haina faida 
Dk 57 sasa, mechi inaonekana kuchezwa kwa tahadhari kubwa, kila timu ikijilinda zaidi na kutaka kupata bao la kushitukiza
SUB Dk 51, Mwinyi Kazimoto anaingia kuchukua nafasi ya Mo Ibrahim
Dk 49 krosi safi ya Massawe lakini juuko anaosha na kuwa kona, inachongwa na Agyei anadaka vizuri kabisa
DK 48 kipa Agyei wa Simba, analazimika kufanya kazi ya ziada kuokoa shuti kali la Jaffar
Dk 45 Kipindi cha pili kinaanza kwa kasi, Simba wakionekana wamepania kuongeza bao la mapema. 
Wanaonekana wakiwa wamebadili jezi na sasa wana zile zenye nembo ya SPORTPESA


MAPUMZIKO
DAKIKA 4 ZA NYONGEZA
Dk 45, Mavugo anabaki yeye na kipa wa Stand ambaye anapangua mpira na kuudaka vizuri
Dk 43, Mavugo anapoteza nafasi nzuri ya kufunga baada ya kichwa chake kutolenga lango
Dk 40, Stand wanaonekana kucharuka na Frank Hamis anapiga kichwa safi kabisa lakinini goal kick
Dk 38, Selembe anapoteza nafasi nzuri akiwa karibu kabisa na kipa Agyei


KADI Dk 37, Frank Hamis wa Stand analambwa kadi ya njano kwa kumzonga mwamuzi akipinga bao. Wachezaji wa Stand walikuwa wanaamini Liuzio alikuwa ameotea 
GOOOOOO Dk 35, Liuzio anaandika bao la pili kwa Simba wakati wachezaji wa Stand wakidhani ameotea
DK 34, kipa Muhonge anaonyesha umahiri wa juu kabisa akidata shuti kali lililolenga lango la Zimber Jr
KADI Dk 31, kipa Muhonge wa Stand United analambwa kadi ya njano kwa kupoteza muda. Awali alionywa kwa maneno
Dk 31, Kichuya tena anapokea pasi sadi ya Mo Ibtra anapiga juuuuu
Dk 30, anaonekana kama mtu fulani asiye makini au uhakika wa anachokifanya. Akiwa na wenzake watatu anajaribu kupiga shuti na linakwenda nje mbali kabisa
Dk 27 Mavugo anaye anaachia mkwaju mkali kabisa, haukulenga lango la Stand, goal kick
Dk 25 Muzamiru anageuka na kuachia shuti kali kabisa, linatoka juu kidogo, goal kick
GOOOOOOOOOO Dk 23, Simba inapata bao la ksuawazisha, krosi safi ya Kichuya na Liuzio anapiga kichwa kuandika bao safi kwa timu yake


Dk 22, Simba inapata kona ya tatu katika mechi hii lakini hana faida
Dk 22 sasa, hakuna mashambulizi makali kutoka upande wowote ule na mpira zaidi unachezwa katikati ya uwanja
Dk 18, Kichua anapata mpira nje ya 18, lakini shuti lake dhaifuuuu
Dk 17, Liuzio anaingia kwa kasi, krosi yake inazuiliwa na kwua kona, inachongwa na Zimbwe, inazuiliwa na kuwa kona tena
KADI Dk 15, kadi ya kwanza ya njano katika mchezo huu inatoka. Anazawadiwa Salamba baada ya kucheza kindava
Dk 12, Muzamiru tena anajaribu hapa lakini halina matumaini


Dk 9, Kichuya naye anaamua kujaribu vizuri hapa lakini kipa Muhonge anadaka vizuri kabisa
Dk 6, nje ya 18, Mzamiru anaachia mkwaju mkali kabisa lakini mpira unaenda juuuuu
Dk 5 Liuzio anaingia vizuri lakini anaukosa mpira katika nafasi nzuri kabisa
DK 3, Kotei anaachia mkwaju mkali wa adhabu lakini mpira unatoka nje
Dk 1, ikiwa ni sekunde ya 18 tu, Selemani Selembe anaifungia Stand bao safi baada ya Kotei kujichanganya na Juuko kushindwa kuokoa

4 COMMENTS:

  1. Tunaomba Lineup ya Stand United

    ReplyDelete
  2. Goli la stand kafunga nani? Acha unazi....

    ReplyDelete
  3. Ya Mnyama yote kafunga Juma Luizio.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic