May 3, 2017

DANTE

Beki wa kati wa Yanga, Andrew Vincent ‘Dante’ amewajia juu mashabiki wa timu hiyo wanaomtupia lawama kutokana na kuizamisha timu katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la FA baada ya kujifunga bao lililowaondosha mashindanoni.


Yanga ambayo wikiendi iliyopita ilitupwa nje ya michuano hiyo kwa kufungwa bao 1-0 na Mbao FC kwenye mchezo wa nusu fainali uliopigwa katika Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, Dante ndiye aliyejifunga bao hilo dakika ya 26.

Taarifa zinasema kuwa Dante amekuwa akipata vitisho na lawama kedekede kutokana na kujifunga bao hilo.
Kutokana na bao hilo, Yanga imejikuta ikishindwa kulitetea taji lake hilo ililolichukua msimu uliopita huku mashabiki na wapenzi wa Yanga wakimtuhumu Dante kuwa ndiye aliyesababisha hayo yote yakatokea.

“Ndiyo imeshatokea ila nimejifunza kwamba kwenye maisha unaweza kukutana na kila aina ya jambo, lakini mwisho wa siku tunatakiwa kukubaliana nalo kwamba ndilo limeshatokea.


“Watu wanaojua soka hawaongei kuhusu mimi ila wale wenye viherehere ndiyo hao wanaoongea vitu wasivyokuwa na uelewa navyo, tunatakiwa kukubaliana kwamba tumeshatolewa katika FA, sasa nguvu zetu zote tunazielekeza katika ligi ambapo ni lazima tuchukue ubingwa,” alisema Dante.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV