Mshambuliaji Donald Ngoma amerejea nchini sasa yuko tayari kuanza mazoezi.
Ngoma alitarajiwa kuanza mazoezi jana au leo na lakini hakuna dalili kama atarejea kabla ya msimu huu kwisha kwa kuwa Yanga imebakiza mechi tatu tu.
Ngoma anasumbuliwa na goti na alikwenda nchini Afrika Kusini kutibiwa na imeelezwa ameshauriwa kupumzika kwa muda kidogo.
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, Salum Mkemi yeye alithibitisha kurejea kwa Ngoma na kusema yuko tayari.
“Anaweza kuanza mazoezi kwa kuwa ametoka kwenye matibabu. Lakini suala la kurudi uwanjani sidhani,” alisema Mkemi.
0 COMMENTS:
Post a Comment