May 3, 2017



Kutokana na Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara kufungiwa na Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF), kutojihusisha na masuala ya soka kwa miezi 12, uongozi wa Simba umekuja juu na kumkingia kifua.

Hivi karibuni, Manara alikumbana na adhabu hiyo kwa kile kilichoelezwa ni kukashifu na kuingilia masuala ya kiutawala ya TFF ambapo mbali na kifungo hicho, amepigwa faini ya Sh milioni tisa.

Evans Aveva ambaye ni rais wa klabu hiyo, amesema: “Wakati msemaji wetu anafungiwa haikuainishwa amefungiwa kutofanya nini, lakini pia siku ya hukumu yeye hakuwepo, hivyo tumeandika barua kuomba hukumu ifanyiwe ‘review’ ili kamati husika isikie utetezi wa mlalamikiwa.


“Hatujaridhishwa na jambo hilo kwani nakumbuka wakati wito umeletwa klabuni ukimtaka Haji aende kwenye kamati hiyo kusomewa mashtaka yake, mimi ndiye niliyepokea barua hiyo na nikaandika barua ya kuwajibu kwamba hawezi kufika kutokana na kuwa likizo, lakini tukashangaa imetoka adhabu bila hata upande wa pili haujasikilizwa.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic