May 3, 2017
Rais wa Simba, Evans Aveva, ameibuka na kusema kuwa, timu yao ilikuwa imejiandaa tangu awali kucheza mechi yao ya fainali ya Kombe la FA katika uwanja wowote hata ingekuwa Nyamagana, Mwanza.

Aveva ametoa kauli hiyo baada ya jana Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitia kwa rais wake, Jamal Malinzi kutangaza mechi ya fainali ya FA kati ya Simba na Mbao itapigwa katika Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

“Tumepata taarifa kwamba tutacheza mechi yetu ya fainali katika Uwanja wa Jamhuri kule Dodoma, sisi hatuna shida yoyote lakini tulishangazwa awali taarifa zilipotoka kwamba itachezeshwa droo kupata uwanja utakaotumika.


“Sisi tulijiandaa kucheza popote pale, hata wangesema CCM Kirumba au Nyamagana kule Mwanza tulikuwa tayari, kikubwa ni kwamba tumejiandaa na hao Mbao watatukuta tayari tumefika Dodoma tukiwasubiri tucheze nao,” alisema Aveva.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV