May 3, 2017



Uongozi wa Klabu ya Simba, umesema kuwa, unasubiri barua kutoka Bodi ya Ligi ili wawasilishe malalamiko yao katika Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) kudai haki yao baada ya kupokwa pointi tatu na Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji.

Simba imefikia hatua hiyo baada ya kamati hiyo kuipoka pointi ilizopewa na Kamati ya Saa 72 baada ya kushinda rufaa yao dhidi ya Kagera Sugar ambayo inadaiwa ilimchezesha beki wake, Mohammed Fakhi akiwa na kadi tatu za njano dhidi yao.

Rais wa Simba, Evans Aveva, amesema njia zipo nyingi za wao kupata haki yao, hivyo wanasubiri kupewa barua kutoka Bodi ya Ligi ambayo wataiambatanisha kwenda Fifa kudai haki yao.


“Kwa kuwa tunasikia kwamba Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji imetupoka pointi zetu tulizopewa na Kamati ya saa 72.

"Tunasubiri kupewa barua rasmi na Bodi ya Ligi kama ilivyotupatia awali ili tuweze kwenda mbele zaidi kudai haki yetu. Tumefuatilia njia za kudai haki yetu tumeambiwa gharama inaweza kuanzia dola 15,000, tupo tayari kulipa ili tupate haki yetu,” Alisema Aveva.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic