May 17, 2017Wazee wa klabu ya Simba wameupongeza uongozi wao chini ya Rais Evans Aveva kufanikisha kupatikana kwa mkataba wa miaka mitano ya kampuni ya michezo ya kubashiri ya SportPesa.

Mratibu wa Baraza la Wazee la Simba, Felix Mapua ameiambia SALEHJEMBE kwamba wanawapongeza kina Aveva na wenzake kwa ubunifu huo.

"Inawezekana kuna sehemu wamekosea lakini inawezekana kurekebishwa. Lakini ukweli ni kwamba sisi tunawapongeza kwa kuwa mkataba huo unapunguza Simba kuendelea kuwa ombaomba.

"Tunachofanya sisi ni kuusihi uongozi endelee kutafuta wadhamini wengine ili kuwa na uhakika wa fedha za uendeshaji wa klabu," alisema.

Simba iliingia mkataba wa miaka mitano na SportPesa kutoka Kenya ambao thamani yake ni Sh milioni 888 kwa mwaka na Sh bilioni 4.9 kwa mwaka.

Lakini taarifa za uhakika ambazo SALEHJEMBE imezipata na kuziripoti ni kwamba, SportPesa wameiongezea Simba mkataba mpya wenye thamani ya Sh milioni 950 kwa mwaka na Sh bilioni 5.173 kwa miaka mitano.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV