May 12, 2017



Klabu ya soka ya Yanga inapenda kuwatangazia wanachama, wapenzi, mashabiki na wadau wa soka jijini Dar es salaam sanjari na mikoa ya karibu kwamba; mchezo wa Jumamosi kati ya Yanga SC  na Mbeya City utachezwa uwanja mkuu wa taifa  kuanza saa 10:30 kama ilivyo ada. 


Maamuzi haya yamezingatia matakwa na masilahi ya wadau wa soka nchini ambao wana kiu na hamu ya kuutazama mchezo huo lakini pia wakiwa ni sehemu ya wadau wa mchezo wa riadha itakayofanyika uwanja wa taifa jumamosi hiyo hiyo. 


Tunawaomba wanachama na mashabiki wajitokeze kwa wingi kuwapa sapoti vijana wao.

Nyote mnakaribishwa

Imetolewa na Idara ya habari na mawasiliano
Young aAfricans Sports Club

12.05.2017

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic