Kampuni kubwa ya michezo ya kubashiri au kubeti ya SportPesa inajulikana kwa udhamini.
Baada ya kutangaza kuingia nchini Tanzania wengi wamekuwa na hamu ya kujua itafanya kipi katika kusaidia michezo kama ilivyofanya nchini Kenya ambako michezo ilikuwa imedorora kabisa lakini sasa mambo ni tofauti baada ya SportPesa kutoa udhamini mkubwa.
SportPesa imezidhamini timu zote mbili kongwe za Gor Mahia na AFC Leopards na maswali mengi hapa Tanzania, wengi wanataka kujua kuhusiana na Yanga na Simba?
Taarifa zinasema hivi, huenda leo ikawa rasmi Simba kuanza kutumia jezi zilizo na nembo ya SportPesa.
Kuna taarifa pande mbili za klabu hiyo kongwe na SportPesa wameishakubaliana na huenda mechi mbili za Simba zilizobaki, wataanza kuvaa jezi za kampuni hiyo.
Kwa Simba itakuwa ni neema na njia mpya ya mabadiliko kwa kuwa wamecheza msimu mzima vifua vyao vikiwa havina mdhamini ambayo ilikuwa ni hasara kwao.
0 COMMENTS:
Post a Comment