May 2, 2017



Yanga ni kama imetuma salamu vile kwa Tanzania Prisons ni baada ya kuishushia kipigo cha mabao 5-0 Buseresele FC ya mkoani Geita.

Timu hiyo, ilipata ushindi huo katika mchezo wa kirafiki uliochezwa kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Waja uliokuwepo Mkoani Geita.
Yanga imeweka kambi Geita kwa ajili ya maandalizi ya mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Prisons itakayochezwa Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. 

Katika mechi hiyo, kiungo mkabaji wa Yanga, Deus Kaseke ndiye aliyefungua pazia hilo la mabao kufunga dakika ya 45.
Mabao mengine yalifungwa na Emmanuel Martin dakika ya 48, 73, Anthony Matheo 89 kabla ya  Amissi Tambwe kufunga la tano.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic