June 1, 2017

DK MWAKYEMBE (KATIKATI) AKIJADILI JAMBO NA ELSTONE WAKATI WAKIWA KWENYE UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR ES SALAAM, LEO.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa klabu ya Everton, Robert Elstone yuko nchini.

Ugeni wa Elstone umeratibiwa na kampuni ya kubashiri ya SportPesa na mgeni rasmi amekuwa ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe.


Elstone, ameongozana na nahodha wa zamani wa Everton, Leon Osman ikiwa ni hatua moja kukaribia ujio wa Everton ambayo itakuja kucheza nchini mwezi ujao.

Uwanjani hapo pia alikuwepo Ofisa Mtendaji Mkuu wa SportPesa Tanzania, Pavel Slavkov.

Bosi huyo wa Everton amepata nafasi ya kuwaona watoto na vijana wa Kitanzania wakicheza soka kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, leo.

Pia anatarajia kuzungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mambo mbalimbali ya maendeleo ya michezo.






0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic