June 1, 2017Bundi wa maisha magumu ameendelea kuzunguka katika mitaa ya Jangwani baada ya wachezaji wake kuanza kulalama chinichini kwamba mshahara sasa umefikia miezi minne.

Wachezaji wa Yanga hawajalipwa mishahara ya miezi minne sasa, jambo ambalo limewafanya waanze kulalamika.

"Kabla ya kwisha kwa ligi, tuliambiwa tupambane kubeba ubingwa. Mambo yatakuwa safi, lakini naona hali si nzuri hadi sasa. 

"Mwisho wa mwezi huu (Mei), itakuwa miezi minne. Mmekuwa mkisema hatujitumi, hatuvumilii. Basi sasa mtutetee, maana miezi minne mingi ndugu zangu na sisi tuna familia," alisema mmoja wa wachezaji wa Yanga.

Viongozi wa Yanga wamekuwa wakikubali kwamba mishahara imekuwa tabu na baada ya kujiuzulu kwa mwenyekiti wao, Yusuf Manji, mambo yamezidi kuwa mabaya zaidi.

Wachezaji hao walipambana mwishoni bila ya mishahara hadi kufanikiwa kufikisha pointi 68 zilizowapa ubingwa kwa tofauti ya mabao dhidi ya Simba.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV