June 24, 2017



Emmanuel Okwi ametua nchini salama salimini.

Kesho itakuwa siku ya kumazana na Simba na baada ya hapo watatangaza rasmi.


Okwi amewasili hivi punde kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) na kupokelewa na Makamu Rais wa Simba, Geofreu Nyange ‘Kaburu’.

Okwi ametua nchini kwa ajili ya kumalizana na Simba na ikiwezekana kusaini mkataba wa miaka miwili.

Mazungumzo ya awali, yamefanyika jijini Kampala, Uganda kati yake na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe.

Kama watamalizana, Okwi anatarajia kusaini kesho na baada ya hapo atarejea Uganda.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic