June 17, 2017


Kikosi cha Monaco ya Ufaransa kimezuua hofu kubwa kwa mashabiki wake.

Mchezaji anayetakiwa zaidi ni Kylian Mbappe, mshambulizi hatari wa kikosi hicho.

Lakini mshambulizi mwingine ambaye Danijel Subasic, Djibril Sidibe, Almamy Toure, Jemerson, Benjamin Mendy, Tiemoue Bakayoko na Thomas Lemar ambao wanaonekana kuzivutia timu nyingi kubwa za Ulaya na kufanya ionekana kama kikosi chote cha kwanza kitanunuliwa.

Kwa hapa Tanzania, mashabiki wa Mbao FC nao wamekuwa na hofu kwa kuwa wachezaji wa kikosi hicho kilichotinga fainali ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Simba, wamekuwa lulu.

Wachezaji hao wamekuwa wakisajiliwa mfululizo na timu mbalimbali kubwa kama Simba, Yanga, Azam FC lakini hata kocha wao pia anaonekana kuwa lulu. Hali inayozua hofu kikosi hicho kukosa nguvu msimu uhao.

Tukirudi kwa mashabiki wa Monaco, nao wameingia hofu kwamba huenda kikosi hicho kikavurugika kabisa kutoka na klabu kadhaa kuwa na nia ya kuwatwa baadhi ya wachezaji.

Kupitia mitandao ya mashabiki wa Monaco ambao wanatambulika na klabu hiyo, wameutaka uongozi kuchukua hatua mapema.

Baadhi ya ushauri wa mashabiki hao ni pamoja na kuwauza wachezaji wao kwa bei za juu ili kupata fedha za kuunda kikosi kipya.

Mashabiki hao wamesisitiza pia wakati mwingine klabu kukataa fedha hizo kama wanaona kuna uwezekano wa kufanya hivyo ili kuepusha Monaco kuvurugika hapo baadaye na hasa msimu ujao.

Monaco ndiyo ilikuwa timu iliyofanya sapraizi kubwa kwa kufika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa na ikapewa nafasi ya kutinga fainali, hata hivyo ilishindwa baada ya kukutana na Juventus iliyokuwa imekamilika.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic