June 26, 2017



Mtibwa Sugar imeeleza kuwa inatarajia kufanya usajili wa nguvu kwa kuwaongeza wachezaji wanne katika nafasi ya ushambuliaji ili kuweza kukiimarisha kikosi hicho kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu.

Mtibwa Sugar ni miongoni mwa timu ambazo wachezaji wake wengi huwa wanachukuliwa na timu mbalimbali za ligi kuu, hivyo safari hii imejipanga kufanya maboresho zaidi.

Kocha mkuu wa timu hiyo, Shabani Katwila, alisema kuwa, kuna wachezaji wanne wamewapointi kutoka timu mbalimbali kwa ajili ya kuongezea nguvu safu yake ya ushambuliaji ambayo ina upungufu.

“Natarajia kusajili washambuliaji wawili na viungo washambuliaji wawili, hivyo jumla nataka kuwa na wachezaji wanne mbele ili kuleta ushindani.

“Kuna baadhi ya wachezaji tunafanya nao mazungumzo kwa ajili ya kuwasajili kutoka timu nyingine ambapo baadhi yao tuliowapointi wameshachukuliwa na timu nyingine.

“Tunahitaji kuimarisha kikosi chetu ili kiweze kuwa na upinzani msimu ujao,” alisema Katwila.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic